Jeshi
la polisi mkoa wa Morogoro limezima maandamano na kuwatawanya kwa
mabovu ya machozi na risasi za mipira wakulima wa vijiji vya kisara
tarafa ya Turiani wilayani Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wakipinga
wafugaji kuingiza mifugo katika mashamba ya wakulima.
Malalamiko hayo ya wakulima yamekuja kufuatia tukio
la ngombe za wafugaji kuuawa ambapo wakulima hao wametupia lawama jeshi
la polisi kushindwa kuondoa mifugo katika maeneo ya wakulima kama
ilivyoagizwa na serikali ya wilaya na kuwatuhumu askari kutumia nguvu
kutawanya maandamano na baadhi ya wakulima kushikiliwa na jeshi la
polisi.
Akizungumzia tuhuma hizo mkuu wa kituo cha polisi
Turia Rajab Shemndolwa amesema wamelazimika kutumia nguvu kutokana na
wananchi kutofuata taratibu za kufanya maandano na kukaidi amri ya jeshi
na kwa kufunga barabara kwa mawe kwa zaidi ya masaa manne na kuzuia
shughuli za usafiri.
Nae mkuu wa wilaya ya Mvomero Antony Mtaka
akizungumzia tuki hilo amekiri uharibifu mkubwa uliofanywa baada ya
mahindi kuliwa na mifugo hali inayosababisha njaa kwa wakulima
waliolima lakini kuwa mkakati wa serikali sasa ni kusikiliza malamiko ya
pande zote mbili katika kutatua mgogoro huo.
CHANZO:ITV
