Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali
Eliezer Feleshi amesema tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa
Uingereza sio la kigaidi.
"matukio haya yasichukuliwe jumla jumla,
sisemi moja kwa moja kuwa tukio hilo ni la kigaidi ila naomba
tuhamasishe jamii ya watanzania utii wa sheria bila shuruti, na tusaidie
vita dhidi ya matumizi mabaya ya tindikali" - Alikuwa anajibu swali
kama tukio la Tindikali nalo ni la kigaidi kama yale aliyopitisha
ofisini kwake yafunguliwe mashtaka ya Ugaidi yaliyokataliwa na Mahakama
IGP- Amekwepa swali la kuwa endapo yupo tayari kujiuzulu kwani matukio mabaya yamekuwa yakiendelea tu.
"Kwanini usijiuzulu kwa kuwa matukio kama haya yamekuwa yakijirudia, na wewe umekalia kiti hicho?"
Hayo yamejiri kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani muda mchache kulikuwa na Press conference, Wazungumzaji walikuwa ni IGP, DPP na Mkemia Mkuu wamechanganyikiwa na tukio la Waingereza kumwagiwa Tindikali. Pamoja na hayo, hoja yangu je Serikali inaamka wageni wakiguswa? tangu lini matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameanza kutokea na serikali haichukui hatua, wala kukamata watuhumiwa.

Mabomu yamelipuka hatujawahi kusikia serikali ikitoa maelezo na namna
ya kujilinda. Leo la tindikali la Waingereza IGP, DPP na Mkemia Mkuu
wanafika kueleza namna ya kudhibiti tindikali, na namna ya kupata
taaarifa za tindikali.