Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
akihutubia Wananchi katika Baraza la Idd lililofanyika Ukumbi wa Salama
Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
=======
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
amesisitiza kuwa Serikali itafanya kila iwezalo kuwakamata na
kuwapeleka katika Vyombo vya sheria Watu waliohusika kuwamwagia
Tindikali Raia wawili wa Uingereza hivi karibuni.
Amesema
Vyombo vya Ulinzi na Usalama viko Imara na kwamba vitaendelea kulinda
amani ya Nchi ikiwemo kuwabaini Wahalifu wote na kuwapeleka katika
Vyombo husika.
Dkt
Shein ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia Wananchi kupitia Baraza la
Idd lililofanyika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
Amesema
kwa mara ya pili kila inapokaribia Sherehe za Sikukuu kumekuwa na
mfululizo wa Matukio ya kihalifu na kuongeza kuwa kila aliyehusika hatua
za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
“Vitendo hivi si uungwa ni Ukatili, hatutawatia hatiani Wasiohusika lakini kila aliyehusika hatutamsamehe” Alionya Dkt Shein.
Aidha
Dkt. Shein amelaani kushamiri kwa Vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia
ikiwemo ubakaji hasa kwa Watoto ambapo jumla ya Watoto wakike 480
Zanzibar wamebakwa katika kipindi cha mwezi Julai 2012 hadi Aprili mwaka
huu.
Amesema hilo ni jambo la kushtua sana na kwamba wakati umefika kila mmoja kuchukua hatua zinazofaa kudhibiti hali hiyo.
Dkt
Shein ametoa wito kwa Wananchi na Viongozi wote kuendelea kupendana
bila kuchukiana na kulinda Amani, Umoja na Kuvumiliana kwa manufaa ya
Zanzibar.
Amesema
panapotokea tofauti za hoja kuhusu suala la Maendeleo ya Nchi jambo la
busara ni kuzungumza na kujadili kwa kuzingatia sheria zilizopo kwa
manufaa ya Zanzibar.
Dkt
Shein ametoa Shukrani kwa Jeshi la Polisi kwa kudumisha hali ya amani
katika kipindi chote cha Mwezi wa Ramadhani na kulitaka Jeshi hilo
lizidishe juhudi zake kipindi cha Sherehe za Idd na siku za usoni.
Kabla
ya Baraza la Idd Dkt Shein alitoa Mkono wa Idd kwa Wazee na Watu
wasiojiweza katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar.