SHEIKH PONDA APIGWA RISASI MOROGORO, SOMA TAARIFA KAMILI HAPA


Muda kama dakika 20 zilizopita mjini Morogoro shehe Ponda amepigwa risasi na polisi .

Dhahama hiyo imempata baada ya kushuka kwenye tax ambako kulikuwa leo akiendesha mhadhala baada ya mhadhala huo kukawa kama kuna maandamano kueleke barabarani, gafla polisi walitokea na kuanza kutawanya wakati huo yeye alikuwa hayupo.


Ndipo muda mdogo akawasili akashuka na ndipo akapigwa risasi.


Haijulikani hali yake. RPC, Faustine Shilogile, anasema hali ni shwari ila Ponda hajui hali yake Maana polisi walizuia gari la Ponda wamkamate, lakini wananchi wakaanza kushambulia polisi ndipo wakarusha risasi hewani kutawanya watu, lakini wananchi wakamtorosha. 

Anasema taarifa ni nyingi za uongo, hakuna watu polisi wala hospitali waliozingira na anaomba anayejua alipo atoe taarifa.

CHANZO:JF


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo