Shehena ya sukari yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisini
iliyoibiwa na majambazi kwa kutumia silaha na kuwakata mapanga kichwani
baadhi ya walinzi katika moja ya ghala ya kuhifadhia bidhaa eneo la
Mbagala rangi tatu jijini Dar es salaam zimekamatwa na jeshi la polisi
huko Chamazi kabla ya kufikishwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa.
Baada ya kupatikana kwa fununu ya kukamatwa kwa shehena ya mifuko
mingi ya sukari, ITV ilitua katika ofisi za polisi wilaya ya Mbagala
maarufu kwa jina la kituo cha Maturubahi ili kujionea ukweli, ambapo
camera ya ITV ilishuhudia lori kubwa yenye namba za usajili T.524 AJZ
aina ya scania ikiwa imepakia mifuko ya sukari ambazo tayari zilikuwa
zimeibiwa usiku wa tarehe 4 mwezi August 2013.
Baada ya ITV kushuhudia mifuko 1312 za sukari, ambayo kila mfuko
ina kilo hamsini, ililazimika kufika eneo la Mbagala rangi tatu
katika ghala ya bwana Haruni Zakaria mmiliki wa kampuni ya Al-Naiem
Enterprises ambapo sukari hiyo ilihifadhiwa na kukuta damu katika
maeneo ambayo walinzi wa ghala hiyo walipigwa na kufungwa kamba kama
anavyoeleza kamanda wa mkoa wa Temeke ACP Englibert Kiondo.
Wakati tukio hilo linatokea baadhi ya majambazi hao walijitahidi
kufanya kila waliwezalo ili kuzimisha sakata hilo,lakini maafisa wa
jeshi la polisi waliamua kusimamia maadili yao ya kazi kwa kukataa
rushwa huku wakiwabana wahusika hao kijeshi ili kutaja mtandao mzima
wanaohusika ambapo maafisa wa jeshi walifanikiwa kufika hadi Chamazi
eneo linalotumika katika kuficha sukari kabla ya kusambaza sokoni.
Kutokana na tukio hilo kuleta hisia kwa wakazi wa maeneo hayo,licha
ya watuhumiwa kumi na mbili kushikiliwa na jeshi la polisi, lakini
baadhi ya mashuhuda walilazimika kutoa maoni yao
chanzo:itv