BARAFU YAWAKOSESHA AJIRA WAFANYAKAZI WA ZAO LA CHAI NJOMBE

Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Ndg.Hosea Mpagike Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capt.Msangi Akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba.
 Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE Capt.Mstaafu Asseri Msangi Akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu Leo.
 
 Mkurugenzi wa Halmashauri Mpya ya Wilaya ya Wanging'ombe Huyu Hapa.
 Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi.Mgeni Baruan Akizungumza Kwenye Kikao cha Kusoma Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu Leo.

Daniel Mwinyi Na Gabriel Kilamlya NJOMBE.

Baadhi ya Wafanyakazi Katika Mashamba ya Chai Mkoani Njombe wametajwa Kukosa Ajira Kutokana na Kuungua na Barafu Zao la Chai Katika Wilaya Mbalimbali za Mkoa wa Njombe

Zao la Chai ni Miongoni Mwa Mazao yanayotegemewa Kwa uchumi wa Mkoa wa Njombe na Taifa Kwa

Ujumla Hususani Katika zao la Biashara na Viazi Mviringo.

Akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010/2015 Awamu ya Nne ya Mwezi Januari hadi Juni Mwaka 2013 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Amesema Kuwa Kutokana na Kuanguka kwa Barafu Nyingi Mkoani Njombe Kumepelekea Kuunguza Mazao ya Chai na Viazi Mviringo Ambayo Tathmini Inaendelea Kufanyika Ili Kubaini Kiasi cha Mashamba yaliyoharibiwa.

Captain Msangi Ameeleza Kuwa  Wilaya zote za Mkoa wa Njombe Zimeathiriwa na Barafu kwenye Mazao ya chai na Viazi Hususani Katika Wilaya ya Makete Ambako Barafu Imekuwa Ikianguka Mara kwa Mara.

Aidha Amesema Kuwa Licha ya Kuwepo na Athari Kubwa ya Mazao Hayo Lakini Bado Hali ya Chakula Imeendelea Kuimarika Kwani Kwa Sasa Zaidi ya Tani Milioni Moja za Chakula zinatarajiwa Kuvunwa na Mazao ya Biashara zikitarajiwa Kuvunwa Zaidi ya Tani Laki Moja.

Pamoja na Mambo Mengine Captain Msangi Amewataka Watendaji wa Halmashauri Pamoja na Madiwani Kuendelea Kuhimiza Juu ya Kujikwamua Kiuchumi kwa Wananchi wao Hususani Katika Sekta ya Elimu,Maji na Umeme.

Jumla ya Vijiji 110 Vinatarajiwa Kupata Nishati ya Umeme Mkoani Njombe Ambapo Hatua Hiyo Itasaidia Kupunguza Adha ya Ukali wa Maisha kwa Kuajiriwa Viwandani na Makampuni Mbalimbali Kupitia Nishati Hiyo.

Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu Iliyosomwa Jana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Imeonesha Dhamira ya Dhati Katika Kuendelea Kupambana na Umasikini Miongoni mwa Wakazi wake Huku Viongozi wakitakiwa Kushirikiana na Wananchi wao Katika Jitihada zaidi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo