
ZAIDI
ya shilingi milioni 41 zimetumika katika shughuli za maendeleo kwa kipindi cha
mwaka mmoja katika utekelezaji wa mpango mkakati wa asasi isiyo kuwa ya
kiserikali ya The Struggle for suppot Community Alliance (SSCSA) Pambana Saidia
Jamii wilayani Kyela
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake leo
mwenyekiti mtendaji wa asasi hiyo Abrahamu Mwanyamaki amesema kuwa
asasi hiyo ilizindua mpango wake mkakati wa miaka mitano februari mwaka jana
ukilenga kutumia zaidi ya bilioni 2 na kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja
wameweza kutumia kiasi hicho cha fedha katika kukamilisha miradi mbalimbali ya
maendeleo
Alisema
kuwa asasi hiyo ambayo usajiri wake ni
wa kitaifa na makao yake makuu yakiwa wilayani Kyela imeweza kufanya upembuzi
yakinifu na kubaini matatizo kadhaa yanayoikabili jamii na kwamba kwa kuanzia
wilayani kyela amebaini kuwapo kwa changamoto kadhaa ambazo asasi yake imeanza
nazo
Alisema
kimsingi huduma za kijamii zinatekelezwa na serikali lakini kutokana na
serikali kuwa na mambo mengi asasi za kijamii kama hiyo uisaidia serikali
katika kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili jamii hii ya Watanzania
Mwenyekiti
huyo mtendaji alisema kuanzia katika kipindi cha Februari hadi Augost mwaka huu
asasi yake imeweza kusaidia kutoa madawati 100 katika shule ya msingi ya
Ikombe,saruji kwa shule ya msingi malungo,mabati katika msikiti mkuu wa
wilaya,mbegu ya matikiti na madawa kwa wajasiliamali wa kata ya Lusungo,Mchanga
kwa ajili ya ujenzi wa hosteli ya walimu kata ya Makwale.
Misaada
mingine ni katika ujenzi wa makanisa na misikiti,kuchangia ununuzi wa vyombo
vya kisasa vya mziki katika makanisa mbalimbali,msaada wa fedha kwa Wahanga wa
mafuriko katika kijiji cha Ngereka kata ya Makwale ambapo mto uliacha njia yake
ya asili na kuharibu makazi ya watu,mashamba na kanisa la KKKT na eneo la
maziko.
Pia
asasi hiyo imefadhili ligi itakayoshirikisha timu mbalimbali katika vijiji na
kata zote za wilaya Kyela na lengo ni kutaka kuifanya jamii kujengeka kiafya na
kuacha kujiingiza katika makundi mbalimbali yasiyofaa na kupata muda wa
kukutana na watu tofauti na kubadiishana mawazo namna ya kujiletea maendeleo
Mwanyamaki
alidai kuwa licha ya kufanya yote hayo lakini amekuwa akikabiliana na
changamoto kubwa kutoka kwa wanasiasa na kuwa shughuli zinazofanywa na asasi
hiyo ni za kijamii na wala haziusiani kabisa na mambo ya kisiasa na kuwa hilo
halitaikwamisha asasi yake kuendelea na shughuli zake za kuisaidia jamii
Na Ibrahim Yassin