Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela, akishiriki kufanya usafi
katika kituo cha zamani cha mabasi mjini Singida ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya sku ya polisi nchini.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela, (wa pili kulia)
akishiriki kufanya usafi katika kituo cha mabasi cha zamani, ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya siku ya polisi nchini. Wa pili kushoto
(aliyeinama) ni RCO mkoa wa Singida Thobias Sedoyeka, akishiriki kuzoa
taka ngumu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya polisi nchini.
Afisa
upelelezi mkoa wa Singida Thobias Sedoyeka, akishiriki kufanya usafi
katika kituo cha zamani cha mabasi mjini Singida, ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya siku ya polisi nchini.(Picha zote na Nathaniel Limu via mo blog).
Na Nathaniel Limu.
Jeshi
la polisi mkoani Singida limeazimisha siku ya polisi nchini kwa kufanya
usafi katika kituo cha zamani cha mabasi mjini Singida.
Akizungumza
na Mo blog, Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey
Kamwela, amesema wameamua kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa jeshi la
polisi kwa kusafisha mazingira eneo la kituo cha mabasi ili pamoja na
mambo mengine, kuondoa uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko.
Akifafanua amesema kuwa mazingira yakiwa machafu, yanasababisha madhara mengi ikiwemo kuficha
Amesema
mazingira machafu yanachangia kutokea kwa milipuko ya magonjwa
yanayoweza kusababisha wananchi wasiweze kujiletea maendeleo endelevu.
Kwa
hali hiyo, Kamanda Kamwela, ametoa wito kwa wakazi wote wa mkoa wa
Singida wakiwemo askari polisi, kuhakikisha mazingira yanayozunguka
makazi yao, yanakuwa safi wakati wote.
Aidha, amesema katika maadhimisho hayo, pia watayatumia katika kujitathmini utendaji wao.
Amesema
baada ya tathimini hiyo, watajiwekea mikakati ya kuboresha utendjai wa
kila siku, ili mkoa wa Singida, uendelee kuwa na amani na utulivu
zaidi.