MTUHUMIWA WA UJAMBAZI ANUSURIKA KIFO KUFUATIA KIPIGO KIKALI CHA WANANCHI KIMARA DAR ES SALAAM


Jambazi akiwa hoi katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kupewa kichapo na wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.

KIJANA mmoja ambaye hajafahamika jina lake anayedaiwa kuwa ni jambazi amenusurika kuuawa na wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi eneo la Kimara jijini Dar es Salaam. 

Kijana huyo akiwa na wenzake wawili waliokuwa na silaha za moto tayari kwa kwenda kufanya uhalifu lakini kabla mpango wao haujakamilika polisi waliingilia kati. 

Haikuwa kazi rahisi kuweza kumkamata jambazi huyo kutokana na majibizano ya risasi kati yao na polisi. Hata hivyo mmoja wao (pichani juu) alitiwa nguvuni wakati wenzake wawili wakitokomea.

(Picha na Khatimu Naheka / GPL)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo