Ikiwa yamepita masaa kadhaa tangu mume wa Joyce Kiria, Bwana Henry Kilewo kuachiwa huru na mahakama kuu kanda ya Tabora baada ya kuona hana hatia, mkewe bi Joyce Kiria ametoa jibu la kitendawili kilichokuwa kikisubiriwa na wengi
kama utakumbuka vizuri wakati mumewe akiwa mahabusu, wadau mbalimbali walimshauri Joyce kuwa mumewe akitoka selo, amshauri aachane na siasa na badala yake afanye shughuli nyingine
Joyce Kiria ametoa majibu ya ushauri huo hii leo muda mchache baada ya mumewe kuachiwa huru, yafuatayo ni aliyoyasema Joyce:-