Mkurugenzi wa shirika la SUMASESU Egnatio Mtawa akitoa maelezo kwa washiriki kuhusu utambulisho wa mradi uitwao "Vijana wa makete na mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi" katika ukumbi wa HIMA Makete wakati wa utambulisho wa mradi huo ngazi ya wilaya leo Augusti 09, 2013. Shirika la SUMASESU ndilo litakalotekeleza mradi huo kwa ushirikiano na UNICEF
Washiriki wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mkurugenzi wa SUMASESU (hayupo pichani)
Mratibu wa ukimwi halmashauri ya wilaya ya Makete CHAC Ester Lamosai(kushoto) akiwa na Anifa Mwakitalima kutoka SUMASESU
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mradi huo ngazi ya wilaya akisikiliza maelezo ya mradi huo kutoka SUMASESU
Mtaribu wa ukimwi sekta ya afya (DAC) Dk Shadrack Sanga akichangia hoja kwenye kikao hicho
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mradi huo ngazi ya wilaya katika ukumbi wa HIMA Makete
Makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Makete Jison Mbalizi akiahirisha kikao hicho