MKENYA ALIYEDHANIWA KUMJERUHI DK ULIMBOKA AACHIWA HURU


Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini Tanzania, Dk Steven Ulimboka.Dar es Salaam, Tanzania. 

JANA, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia mashtaka raia wa Kenya,  Joshua Mulundi, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kumteka na kumjeruhi Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini  Tanzania, Dk Steven Ulimboka.

Hakimu Warialwande Lema aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo alifikia hatua hiyo baada ya Mkurugenzi wa Mashtka nchini (DPP) kuwasilisha hati ya kumfutia mashtaka hayo.

Hati ya DPP kumfutia mashtaka hayo mshtakiwa huyo, iliwasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Beatha Kitau, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi umekamilika.

Katika shambulio hilo Dk Ulimboka alijeruhiwa vibaya sehemu ya kichwani na maeneo mengine ya mwili na kulazwa katika Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu.

Baada ya kutibiwa kwa muda mfupi katika hospitali ya Muhimbili Dk Ulimboka alipelekwa Afrika Kusini kwa Matibabu zaidi.

NA HABARIMASAI BLOG


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo