Wakazi
wa kijiji cha kiwere na Kipera vilivyopo kata ya Karenga wilaya ya
Iringa wakitembea juu ya kivuko chao cha miti cha muda baada ya kivuko
chao kuondolewa na maji,aidha Wakazi hao wanalazimika kutembea umbali wa
km 50 baada ya daraja la mti kuzolewa na maji.
==========
WAKAZI wa
kijiji cha kiwere na Kipera vilivyopo kata ya karenga wilaya ya Iringa
wanalazimika kutembea umbali wa km 50 baada ya daraja la mti kuzolewa na
maji.
Akizungumza
mwenyekiti wa kijiji cha kiwere,Yustin Lipita alisema kuwa kutokana na
ubovu wa daraja ambalo linaunganisha vijiji hivyo viwili wanakijiji hao
wanalazimika kutembea umbali mrefu ili kufuata zahanati ya serikali
ambayo ipo katika kijiji cha kipera .
“tunaiomba
serikali kutujengea daraja ili wakazi wa kiwere na kipera waondokane na
adha ya kutembea umbali mrefu kupitia Mlambalasi mpakani mwa Tarafa ya
Pawaga na Kalenga palipo na umbali wa klm.46 kufuata shughuli zao za
kilimo pamoja na huduma muhimu za kijamii”alisema Lipita.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kijiji cha kipera Bonifasi Mgomati alisema
kuwa Changamoto nyingi zimejitokeza kutokana na ubovu wa kivuko hicho ni
vifo vya wakazi wa vijiji hivyo pamoja na kupoteza vitu vingi kama
mizigo na Baiskeli kuendana maji.
“Ni
kivuko cha mudamrefu katika eneo hili toka mwaka 1975 Ingawa kabla ya
hapo ilitumika kamba ya katani iliofungwa Ng’ambo na Ng’ambo na mvukaji
kuitegemea anapovuka “alisema mgomati.
Sambamba
na hayo mkazi mmoja wa kijiji cha kipera Antoni Kigehe alisema
wanalazimika kutumia kivukohicho wanapokwenda katika Mashamba yao
yaumwagiliaji yaliopo kijiji cha Kiwere jambo ambalo ni hatari kutokana
na mazingira ya Daraja hilo la Miti pia ni vigumu watoto wadogo kuvuka
pekeyao kwakuhofia usalama.
CREDITS: JIACHIE