MATUMAINI AWASHUKURU WASANII WENZAKE KUMNUSURU NA KIFO

 
BAADA ya kutoka nchini Msumbiji akiwa hoi, msanii wa vichekesho Bongo, Tumaini Mwakibibi Matumaini hatimaye amepata nguvu na ameanza kujikongoja katika kazi ya uigizaji. 

Akichonga hivi karibuni, Matumaini alisema kwa sasa anaendelea vizuri na ameshaanza kucheza filamu mbalimbali anazoshirikishwa na wasanii wenzake na sasa anaendesha maisha yake mwenyewe. 

Nawashukuru sana wasanii wenzangu kwani kama siyo wao, ningerudishwa nikiwa maiti, sina cha kuwalipa ila Mungu ndiye atakayewalipa, alisema Matumaini. 

Hata hivyo, alilaani vikali baadhi ya wasanii wanaozusha maneno ya uongo kwamba Michael Sangu alikula fedha alizokuwa anachangisha kwa ajili yake jambo ambalo siyo la kweli.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo