
Mganga
mfawidhi wa Hospitali ta Wilaya ya Tunduru Dkt. Joseph Ng'ombo
akimuangalia mtoto huyo aliyezaliwa akiwa hana macho, pua na Shavu
linalo shika mdomo wa juu, kushoto ni mkunga wa zamu katika Hospital
hiyo Rukia Nguo akiwa akiwa amekishika kichanga
=======
MAJONZI na
Simanzi zilitawala kwa wanafamilia na Wauguzi katika hosipitali ya Wilaya ya
Tunduru baada ya ndugu yao mkazi wa Kijiji cha Kadewele Mjini hapa
aliyetambuliwa kwa jina la Rehema Safi (42) kujifungua Mtoto wa ajabu mbaye
pamoja miongoni mwa maajabu hayo nipamoja na kuzaliwa akiwa na Jinsia Mbili.
Kichanga hicho ambacho kimezaliwa kikiwa na uzito wa kilo 1.8 pia kimezaliwa
kikiwa hakina Pua,macho na Shavu ambalo hushikilia mdomo wa juu.
Tukio hilo
ambalo lilisababisha mshtuko na taaharuki kwa wataalamu wanaotoa huduma ya
kiafya limetokea katika Hospitali ya serikali ya Wilaya ya Tunduru Mkoani
Ruvuma Agosti 5 mwaka huu.
Mkunga wa
zamu katika Wodi ya wazazi iliyopo katika hospitali hiyo Rukia Nguo alisema
kuwa pamoja na uzoefu wake wa muda mrefu katika kada hiyo hajawahi kuona
kiumbe cha aina hiyo.
Alisema
baada ya tukio alilazimika kuwaita waganga na wauguzi wenzake ili wamsaidie
kutazama kichanga hicho ili kujiridhisha juu ya tukio hilo akidai kuwa awali
akiwa peke yake akishindwa kukitambua kiumbe hicho kama ni binabamu ama la
ingawa kilionekana kuwa na viungo vingine vya kibinadamu.
Kufuatia
hali hiyo Mkunga huyo alitoa wito kwa wanawake wenzake kuachana na
tabia ya kutumia dawa za kienyeji na badala yake waende hospital kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa maafisa
tabibu
“unajua sisi
wanawake wengi tumekuwa na tabia ya kuchukua na kuanza kuzitumia dawa kutoka
kwa ndugu jamaa na marafiki “ alisema Nguo na kuongeza kuwa matumizi ya dawa za
aina hiyo zinaweza kusababisha madhara makubwa yakiwemo yanayo sababisha
kuzaliwa kwa watoto wenye upungufu wa viungo.
Akizungumza
kwa unyonge juu ya tukio hilo mama mzazi wa Mtoto hoyo ambaye hadi sasa
hajapatiwa jina, Reheme Safi ambaye uzazi huo ni wa tano alisema kuwa hana budi
kulipokea tukio hilo kama changamoto ya maisha kwani mtoaji nimungu na kwa
hatua hiyo hawezi kubishana na uumbaji huo.
Mganga
Mfawidhi wa hospitali ya serikali ya Wilaya ya Dkt. Joseph Ng’omboa
amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa maafisa tabibu wanaendelea
kufanya utafiti wa chanzo cha tukio hilo kwa kumpima mama huyo kama ana
magonjwa ya kuambukiza ama la.
Alisema
mtoto kuzaliwa akiwa katika hali hiyo kunaweza kusababishwa na mambo mengi
yakiwemo magonjwa ya zinaa, kukosekana kwa virutubisho Fulani wakati wa
uumbwaji wa viungo mwilini ama mama mzazi kutumia madawa wakati akiwa na mimba changa.
Aidha Dkt.
Ng’ombo pia alitumia nafasi hiyo kuwahamasisha akina mama wajawazito kuhudhulia
Kliniki katika kipindi chote baada ya kupata ujauzito na kwenda kujifungulia
hospitali kwa ajili ya kupata msaada wa maafisa tabibu wakati wote.
CHANZO:FREEBONGO