Hatimaye Mansoor Yussuf Himid, mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki mjini
Unguja, amekubali kufanya mazungumzo yake ya kwanza na Idhaa ya
Kiswahili ya DW tangu uamuzi wa Chama chake cha Mapinduzi wa kumvua
uanachama.
Kwa mujibu wa taarifa ya CCM kwa vyombo vya habari ni
kwamba Mansoor amevuliwa uwanachama baada ya kukiuka miiko ya chama
hicho tawala nchini Tanzania, hasa kwenye suala la muundo wa Muungano.
Katika mazungumzo haya na Sudi Mnette, kwa
mara ya kwanza mwansiasa huyo kijana, ambaye hapo jana Halmashauri Kuu
ya CCM ilitangaza kumfukuza chamani, ameeleza baadhi ya yale yaliyo
moyoni mwake.
Kusikiliza mahojiano kamili, tafadhali bonyeza hapa chini.