FILAMU IITWAYO SHAHAADA NI ZAIDI YA FILAMU YA TOBA

Issa mussa
Cloud 112 mwigizaji na muongozaji wa filamu Swahilihood.

MUONGOZAJI na mwigizaji mahiri wa filamu ambaye pia ni mtayarishaji Issa Mussa ‘Cloud 112’ amesema kuwa filamu yake iliyotoka hivi karibuni ya Shahaada ni filamu bora kuliko kazi yake aliyoitoa siku za awali ya Toba, filamu hiyo ambayo ilitoka siku ya Ijumaa iliyopita imepokelewa vizuri na wapenzi wa filamu Swahilihood kiasi hata cha kumpa hamasa kutengeneza filamu kali zaidi.

Issa Mussa
Cloud 112 akiwa katika moja ya scene za filamu ya Shahaada.
IssaMussa
Cloud112 akiwa katika sehemu ya filamu hiyo
Shahaada
Filamu ya Shahaada

“Natumia muda mwingi sana katika kutafitii kuhusu kazi ninayotaka kuifanya kwa ajili ya wapenzi wa kazi zangu ndio kila ninapotoa kazi mpya lazima ipokelewe vizuri na wadau wa filamu jambo ambalo kwangu ni furaha na ninashukru kwa kupokelewa vizuri filamu ya Shahada wasanii walioshiriki wamefanya vizuri, kazi hii inaizidi Filamu yangu ya Toba,”anatamba Cloud 112.

Filamu ya Shahada imebebwa na wasanii kama Richard Mshanga ‘Masinde’ Esha Buhet, Salama Salmin ‘Sandra’, Awadh Salehe, Skyner Ally Cloud 112 na wengine kupitia kampuni yake mahiri ya utengenezaji wa filamu ya Cy&Cl ndio iiliyofanikisha utengenezaji wa kazi bora ya Shahada na kusambazwa na klampuni ya usambazaji wa filamu Bongo ya steps Entertainment.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo