Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao maalum cha
Kamati Kuu ya CCM, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma leo, Agosti 25,
2013. Kikao hicho kilifanyika kwa ajili ya kukutana Mbunge wa Bukoba
mjini Khamis Kagasheki, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera, Constansia
Buhiye, Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Abedi Mushi, Mwenyekiti na Katibu
wa CCM wilaya ya Bukoba mjini na Meya wa Manispaa ya Bukoba Anatory
Amani kuhusu sakata la madiwani wa wanane wa CCM katika Manispaa ya
Bukoba mjini. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Constansia Muhiye na Katibu wa CCM wa
mkoa huo, Abedi Mushi wakisubiri kuingia ukumbini kukutana na Kamati kuu
mjini Dodoma leo.
Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki akiwasili Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Kagasheki akiperuzi mtandao wakati akaisubiri kukutana na Kamati Kuu mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Bukoda akiingia ukumbini
Kagasheki akiingia ukumbini
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Mwana-CCM
mwenye ulemavu wa miguu, Shija Luhende kutoka Mwanza, ambaye alimkuta
kwenye viwanja vya Makao Mkuu ya CCM mjini Dodoma leo, akitafuta msaada
wa baiskeli.
Nape akimsikiliza kwa makini mwana-CCM huyo
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya
CCM, Abdallah Bulembo akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,
Jenista Mhagama, nje ya ukumbi, Makao Mkuu ya CCM mjini Dodoma, leo.PICHA KWA HISANI YA CCM
KAMATI KUU YAKUTANA NA KINA KAGASHEKI, NAPE AZUNGUMZA NA MWANA-CCM MWENYE ULEMAVU DODOMA
By
Edmo Online
at
Sunday, August 25, 2013





