CUF YAMTAKA RAIS KIKWETE KUVICHUKULIA HATUA VYOMBO VYA DOLA

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/04/166.jpg
Profesa Ibrahim Lipumba
 Sheikh Ponda baada ya kujeruhiwa

Chama cha wananchi CUF kimemuomba rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua hatua juu ya vyombo vya dola vinavyoendeleza tabia ya kutumia vyombo vya moto kukabiliana na raia na kusababisha majeraha na hata kupelekea mauaji ya raia kwa kigezo cha kulinda amani.
 
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa sheikh Ponda Issa Ponda huko mjini Morogoro.

Aidha Profesa Lipumba amesema amefanikiwa kwenda kumuona katika hospitali ya taifa Muhimbili na kusema amepigwa risasi bega la kulia.
 
CHANZO:ITV


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo