BINTI WA MIAKA 14 AJIFUNGUA MAPACHA WATATU

Mmoja wa mapacha wa Mwanarahab Wamukoya.

BINTI wa miaka 14, Mwanarahab Wamukoya wa Bungoma nchini Kenya jana usiku alijifungua mapacha watatu.

Kwa sasa binti huyo na wanaye hao wa kiume wapo hospitali na hali zao ni nzuri.

Mwanarahab aliwashagaza wafanyakazi wa hospitali ya wilaya Bungoma siyo kwa kujifunga mapacha watatu bali umri mdogo wa miaka 14 alionao.

Mama wa mapacha hao watatu anaeleza kuwa yeye pamoja na baba watoto wake mwenye umri wa miaka 16 walitaka kuoana baada ya kupata ujauzito huo lakini mpango wao haukufanikiwa.

Madaktari katika hospitali hiyo wamefurahi kwa kitendo alichokionyesha Mwanarahab kwenda kujifungua hospitali na hakufanya kama mabinti wengi wanaopenda kujifungulia nyumbani.TAZAMA VIDEO YAKE HAPO CHINI

CREDIT: KTN


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo