Sheikh Ponda Issa Ponda akifikishwa mahakamani akiwa chini ya ulinzi.
Sheikh Ponda akiwa kizimbani leo.
Sheikh Ponda akirudishwa kwenye Karandinga baada ya kesi yake kuahirishwa.
Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro kujibu mashitaka yanayomkabili.
Sheikh Ponda amepandishwa kizimbani na kusomewa upya mashtaka matatu, ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 11 mwaka huu na uamuzi kuhusu dhamana ya kesi yake kujulikana Septemba 17
(PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE GPL, MOROGORO)