AJALI YA GARI YAUA 13 NA WENGINE 11 WAKIJERUHIWA SHINYANGA

Habari za kusikitisha ambazo zimetufikia hivi punde zinasema jumla ya watu 13 wamefariki dunia usiku wa kuamkia hii leo huku 11 wakijeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Hiace kutoka kijiji cha Ngogwa wilayani kahama kwenda ushirombo mkoani Shinyanga kugonga lori kwa nyuma usiku wa kuamkia hii leo.
 
Akizungumza na mwandishi wetu Reuben Mchome wa MCHOME BLOG kaimu kamanda wa pilisi mkoani shinyanga kamishna msaidizi wa polisi KIHENYA KIHENYA amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva gari lililokuwa limewabeba abiria hao aina ya Toyota Hiace kuligonga kwa nyuma lori lililokuwa limepaki pembeni kidogo ya barabara ambalo lilikua limeharibika.

Watu watatu kati ya 11 waliojeruhiwa wapo mahututi katika hosiptali ya mkoa wa shinyanga na ni watu wanne tu waliotambuliwa kati ya 11 waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Chanzo:MCHOME BLOG


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo