ZAHANATI YAFUNGWA KWA SIKU KADHAA MKOANI NJOMBE KWA KUKOSA WATAALAMU



MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE KASKAZINI DEO SANGA AKIONGEA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA IKONDO LEO KIJIJINI HAPO.
 
Na Michael Ngilangwa.
Zahanati ya Kijiji cha Ikondo katika kata ya Ikonda wilayani Njombe imesimama kufanya kazi kwa muda wa siku ya mbili sasa baada ya wauguzi na wakunga wa zahanati hiyo kufunga na kwenda kwenye semina mjini Njombe ambapo pamoja na mambo mengine wagonjwa wa kijiji hicho wapo hatarini kupoteza maisha kwa kukosa huduma za matibabu.

Wakizungumza Mbele ya Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini Bwana Deo Sanga wananchi wa kijiji cha Ikondo wamelalamikia kufungwa kwa
zahanati hiyo kutokana na kile kilicho daiwa kuwa madaktari wamekwenda kwenye semina tangu jana Julai 23 huku wagonjwa wakiachwa pasipo kupatiwa huduma za

matibabu.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa katika zahanati hiyo wanakabiliwa na changamoto mbali,mbali ikiwemo ya ukosefu wa nyumba za waganga,ukosefu wa dawa zikiwemo za kuvubaza makali ya virusi vya UKIMWI na kwamba kwa sasa wanasafiri umbali wa zaidi ya kilomita 50 kwenda kupata tiba hiyo kutokana na zahanati hiyo kuwa haina uwezo wa kutoa huduma hiyo.

Akizungumzia tatizo la kufungwa kwa zahanati hiyo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Filbert Mbwiro amesema kuwa amesikitishwa na kitendo cha kufungwa kwa zahanati hiyo na kwamba ni kinyume cha sheria kwa watumishi wa afya kufunga zahanati na kuondoka wote kuelekea kwenye semina na kwamba atalifuatilia halmashauri kujua aliyetoa barua ya kwenda kwenye semina kwa watumishi na kufunga zahanati hiyo.

Aidha bwana Mbwiro amesema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa watumishi hao mara tu itakapobainika wameondoka pasipo utaratibu na kuwataka radhi wananchi kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki wakati taratibu za kuwatafuta wauguzi hao ili kuendelea kutoa huduma zikiendelea katika zahanati hiyo.

Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini bwana Deo Sanga amemuagiza kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe kuhakikisha zahanati hiyo inafunguliwa mapema iwezekanavyo na kwamba watumishi 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo