WATUMISHI WA SERIKALI WILAYANI MAKETE MATATANI KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA

 
Mahakama ya wilaya ya Makete.

Mahakama ya wilaya ya Makete imewaachia kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana watuhumiwa wawili wanaodaiwa kupokea rushwa

Watuhumiwa hao ambao ni askari polisi wa kituo cha polisi Matamba wilaya ya Makete PC Richard Mwanisawa(25) mwenye namba G6094 na mtuhumiwa mwingine ni Thomas Mgerifyamba (55) mlinzi wa idara ya mahakama wilaya ya Makete ambapo wanashtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa mtandao huu na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Makete imeeleza kuwa mtuhumiwa Richard Mwanisawa anatuhumiwa kushawishi na kupokea rushwa ya sh. 50,000/= na Thomas Mgerifyamba anatuhumiwa kushawishi na kupokea rushwa ya sh. 100,000/= kinyume na sheria ya rushwa kifungu namba 15(1)A ya mwaka 2007

Taarifa hiyo iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Makete Daudi Ndyamukama ofisini kwake imesema PC Richard alifikishwa mahakamani na Takukuru Julai 12 mwaka huu ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 30 mwaka huu huku Mgerifyamba alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Julai 26 mwaka huu na kesi yake itatajwa tena Agosti 26 mwaka huu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo