Zaidi ya shilingi milioni 8 zimepatikana katika harambee ya kuchangia sehemu ya mradi wa ujenzi wa nyumba mpya ya kulala wageni inayotarajiwa kugharimu sh. milioni 150 katika kituo cha Udiakonia Tandala kilichopo kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe mwishoni mwa wiki
Kituo hicho ambacho kipo chini ya kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya kusini kati kimefikia hatua hiyo kama njia mojawapo ya kujipatia mapato ili kiweze kujiendesha chenyewe
Mgeni rasmi katika harambee hiyo mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk. Norman Sigala alichangia kiasi cha shilingi milioni 2 kutokana na kuona umuhimu wa mradi huo ambao unatarajiwa kuwa chachu ya maendeleo ya kituo hicho
Dkt Sigala pamoja na mambo mengine pia amewaasa viongozi wa dini kutojihusisha na masuala ya kisiasa kwa kuwa dini na siasa havikai pamoja na matokeo yake kutaliletea matatizo taifa letu
"Ndugu zangu, dini na siasa haviendani kamwe viongozi wa dini nawaomba msijihusishe na masuala ya siasa kwani hayakai pamoja, ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima hapa nchini" alisema Dk sigala
Kwa upande wake Katibu wa kituo hicho mdiakonia Elikana Kitahenga ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya makete ambao wanafanya kazi nje ya wilaya hiyo kuona umuhimu wa kuchangia shughuli za kiamendeleo katika wilaya hiyo kwa kuwa hakuna atakayefanya maendeleo kwenye wilaya yao isipokuwa wao wenyewe
Amesema wilaya hii pamoja na kujengwa na watu wengine lakini zaidi maendeleo yatafanywa na wanamakete wenyewe bila kujali wapo ndania ama nje ya wilaya hiyo
Na Ergon Sanga