BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya
ya Kalambo mkoani Rukwa, wametaka katika katiba ijayo kuwe na muundo wa
Serikali moja, huku Zanzibar ikiwa ni moja ya mikoa ya nchi ya Tanzania
na iwapo Wazanzibari watakataa, waruhusiwe kujitenga.
Mmoja wa wajumbe wa baraza hilo la Katiba Wilaya
ya Kalambo, Afred Ntinda mkazi wa kata ya Mwazye kijiji cha Mpenje
alisema hayo jana wakati akichangia maoni katika kikao cha baraza hilo
kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya mjini hapa.
Mpenje alisema kuwa mfumo wa sasa wa Serikali
mbili una kasoro nyingi na umeshindwa kutatua kero za Muungano hivyo
hautakiwi kuendelea kuwepo wakati ule wa Serikali tatu hawezi kulinda
muungano huo kwa kuwa Serikali hizo zinaweza kuongozwa na marais kutoka
vyama tofauti vya siasa na wenye mitizamo isiyolingana hivyo kuna hatari
ya muungano kuvunjika.
“Sisi huku bara kuwa na Serikali moja si tatizo
wengi wataridhia, nafikiri kuna tatizo katika upokeaji wa maoni kwa
wenzetu wa Zanzibar.