MWANAFUNZI AFUNGWA MIAKA 35 JELA BAADA YA KUMBAKA MWANAFUNZI MWENZIE TANGA


Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Komnyang'anyo wilayani Handeni mkoani Tanga, Mustafa Athumani (18) amehukumiwa miaka 35 jela baada ya kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi mwenzake wa shule ya msingi.

Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya Handeni, Patrick Maligana amesema ameridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka zikiwamo nyaraka zinazothibitisha kwamba Amina ana mimba.
 
Nyaraka hizo ni kadi ya kliniki na barua kutoka kwa mkuu wa shule zinazothibitisha Amina alikuwa mwananfunzi wa shule hiyo ila aliacha kwasababu ya ujauzito.
 
Mahakama hiyo ilielezwa kwamba Disemba 2011 mpaka Juni 2012, mshtakiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Amina Adamu (14) ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi, Msasa na kumsababishia ujauzito na kuachishwa shule akiwa darasa la sita.

Hakimu Maligana alifafanua kuwa sheria inatambua kuwa iwapo mtu yeyote atafanya mapenzi na msichana aliye chini ya umri wa miaka 18 hata kama ni urafiki wa makubaliano kwa sheria za Tanzania mtu huyo atakuwa amebaka.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo