MWENYEKITI WA KIJIJI AMUUA MKEWE KWA KUMNYONGA SHINGO HUKO KAHAMA

 
IGP Said Mwema.
 

MWANAMKE mmoja aitwaye Nyamizi Elias Salamba mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa kijiji cha Ilomelo kata ya Ulowa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, ameuawa kwa kunyongwa shingo na mwanamme anayedaiwa kuwa ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kasela wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limesema tukio hilo limetokea Jumapili ya wiki iliyopita katika kijiji cha Ilomelo wilayani Kahama majira ya saa nne usiku ambapo mwanamke huyo alinyongwa shingo na hawara yake aliyejulikana kwa jina la Kashindye Abeid Sheni mwenye umri wa miaka 45 ambaye ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kasela kilichopo mkoani Tabora.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Evarist Mangalla alikitaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni wivu wa mapenzi baada ya marehemu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamme mwingine ambaye hajafahamika, kitendo ambacho kilimuudhi Mwenyekiti huyo.

Kamanda Mangalla alisema mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo