Wataalamu wa vyombo vya udhibiti wa vyakula na dawa feki katika nchi
16 mashariki na kusini mwa Afrika wamekutana jijini Dar es Salaam
kujadili changamoto na kuweka mfumo wa pamoja chini ya uratibu wa
shirika la afya duniani unaolenga kuliepusha bara la Afrika kugeuzwa
dampo la bidhaa feki duniani.
Kwa mujibu wa taarifa ya meneja wa mradi wa udhibiti kutoka makao
makuu ya shirika la afya duniani yaliyopo Geniva nchini uswis Bw.
Michale Deats amesema mkutano huo wa siku tatu mbali na kujadili
changamoto za udhibiti pia mkutano huo utaweka mikakati shirikishi ya
kuhakikisha Afrika inafunga njia zote za uingizaji bidhaa za aina hiyo
kwa usalama wa afya za binadamu huku akifafanua tatizo hilo na hatua za
udhibiti katika eneo la Afrika na dunia kwa ujumla.
Awali katika taarifa ya mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya chakula a
dawa nchini tfda bw. Hiit sillo pamoja na kueleza hatua za mamlaka
katika udhibiti alipongeza shirika la afya duniani who kwa kuiteuwa
tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo muhimu akieleza fulsa hiyo
kuchochea mikakati ya mamlaka na taifa katika kudhibiti uingizaji wa
vyakula na dawa vilivyopo chini ya kiwago.
Mkutano huo ulifunguliwa na naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii
dk. Seifu rashidi akijipambanua kuchukua hatua kali dhidi ya wanaokiuka
taratibu na wakati huo akijikuta katika wakati mgumu kujibu maswaili ya
waandishi wa habari yaliyomtaka kueleza hatua zilizochukuliwa dhidi ya
mmiliki wa kiwanda kilichothibitika kutengeneza Arv feki na kuelekeza
lawama zake kwa mkurugenzi wa mashtaka dpp anayemtaja kutambua wajibu
wake.
NA ITV