Rais Jakaya Kikwete na waziri mkuu wa serikali ya Thailand bibi
Yingluck Shinawatra wameshuhudia utiliaji saini wa hati nne za
makubalino ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ikiwemo makubaliano ya
kuhamisha wafungwa pamoja na ushirikiano katika teknolojia.
Tukio hilo limetokea Ikulu jijini Dar es Salaam,baada ya kiongozi
huyo wa ngazi ya juu wa serikali ya Thailand kuwasili Ikulu jijini Dar
es Salaam na kupokewa na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete huku zaidi ya
wanawake 200 wakiwa wamejipanga mistari kuelekea Ikulu wakipungia kwa
bendera za Tanzania na Thailand ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kiongozi
huyo.
Katika hati ya makubaliano ya kwanza, mbele ya viongozi hao,
mwakilishi wa serikali ya Thailand ametiliana saini na kukabirishana
hati na naibu waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa Pereira Silima kuhusu
kuhamisha wafungwa, ambapo waziri wa fedha na uchumi mheshimiwa Dkt
William Mgimwa amesaini hati mbili za makubaliano ya kuhamasisha na
kulinda uwekezaji pamoja na ushirikiano wa teknolojia kati ya nchi hizo
mbili.
Ambapo katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini bwana Eliakim
Maswi amesaini hati ya makubaliano ua ushirikiano na mkurugenzi mkuu wa
taasisi gm ya nchini Thailand katika maswala ya nishati na madini.
Bibi Yingluck Shinawatra yuko nchi kwa ziara ya siku tatu ya
kiserikali ambapo akiwa hapa nchni anatarajiwa kutoa msimamo wa nchi
yake kwa bara la Afrika,kabla ya kuondoka jijini Dar es Salaam kuelekea
katika mbunga ya wanyama ya Serengeti ambapo akiwa huko atasaini hati
makubalinao ya ushirikiano wa mbuga za wanyana na umiliki wa wanyamapori
kati ya Tanzania na Thailand, tarehe 1 Agosti anatarajiwa kuondoka
nchni kuelekea Entebe nchni Uganda.