Vifusi hivyo vikiwa barabarani
Greda likianza kusambaza vifusi hivyo jana saa 10 jioni.
Ukaaji
wa vifusi vilivyolundikwa katika barabara ya Sunji – Lupila kwa takribani mwezi
mmoja bila kusambazwa umelalamikiwa na wafanyabiashara waliofika mnadani Lupila
wilayani Makete mkoani Njombe kutokana na kupata adha kubwa wakati
wakisafirisha bidhaa zao
Hayo
yamesemwa na wafanyabiashara hao wakati wakizungumza na waandishi wa habari
mnadani hapo na kuitaka serikali kulirekebisha hilo mapema ili iwe rahisi kwao kuleta tena
bidhaa mwezi ujao
Mfanyabiashara
wa mitumba Mama Mwalukisa amesema kutokana na wao kutumia magari makubwa
kusafirisha bidhaa hizo, magari hayo yammewapa tabu kubwa barabarani kutokana
na kukwama kwenye vifusi hivyo ilihali huu si msimu wa masika
“Yaani
kwa kweli kama tungejua barabara iko hivi hata tusingekuja, magari haya
tumekodi halafu tunajua barabara ni nzuri lakini kwa hali hii kwa kweli hapana,
tunatoa wito kwa serikali irekebishe hii barabara kabla yam nada ujao wa mwezi
Augusti kama wanataka tuje tena” alisema Mama
Mwalukisa
Amesema
kutokana na magari hayo kukwama mara kwa mara kwenye vifusi na wakati mwingine
gari kulala, kumemwogopeha na kuzaimika kuteremka na kupanda kwenye gari la
abiria ili kuondokana na kero ya kuhofu mara kwa mara
Naye
mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Njombe ambaye alikuwepo mnadani hapo Bi
Nesfaneti Digati amesema ni muda wa serikali kutatua kero hiyo mara moja kwa
kuwa lengo la wafanyabiashara hao ni kuleta huduma kwa wananchi tena kwa bei
nafuu
Akizungumzia
kero hiyo diwani wa viti maalumu tarafa ya Ukwama (kata ya Lupila ikiwemo) Bi
Lenesta Lwila amekiri kuwepo kwa kero hiyo na kusema wao kama
madiwani wamemwagiza mhandisi wa wilaya kuona uharaka wa kusambaza vifusi
hivyo, lakini kabla ya kufanya hivyo greda la halmashauri ambalo lingetumika
kwa kazi hiyo limeharibika na lipo katika matengenezo
Amesema
mbali na hivyo wanawasiliana na mhandisi kuona nini wakifanye ili kutatua
tatizo hilo na anaimani kuwa vitasambazwa kabla
ya mnada ujao na wakija tena mara nyingine watakuta barabara iko safi
Hata
hivyo mtandao huu umekuta zoezi la kusambaza vifusi kuanzia Maliwa hadi Lupila
ukianza, ambapo mwandishi wetu ameshuhudia usambazaji wa vifusi ukuanzia Maliwa