Wananchi
wa kata ya Lupila wilayani Makete mkoani Njombe, wameipongeza halmashauri ya
wilaya ya Makete kwa kuanzisha kwa mara ya kwanza mnada katika kata hiyo ambao
umewaletea unafuu wa bei za mahitaji mbalimbali waliyoyapata mnadani hapo
Wakizungumza
na mwandishi wetu wananchi hao wamesema kwa mara ya kwanza mnada huo kufanyika
katani hapo, ambapo wengi wao wamejipatia mahitaji mbalimbali ambayo walikuwa
wakiyafuata mbali na kulazimika kununua kwa bei kubwa
Bw.
Aldo Sanga amesema bidhaa kama nguo walikuwa
wakienda kuzinunua Ikonda ama mkoani Njombe umbali wa zaidi ya kilomita 50 na
hivyo kulazimika kulipa nauli kubwa lakini kunapokuwepo na mnada bei hupungua
“Mfano
hapa Lupila mche wa sabuni huuzwa shilingi 1500 kwenye maduka lakini leo
nimenunua hapa mnadani kwa sh. 1000 kwa mche mmoja, sasa huu si unafuu kwetu
Kwa
upande wao wafanyabishara wameitaka halmashauri ya wilaya ya Makete kuongeza
kasi ya kutangaza minada hiyo kupitia vyombo vya habari na viongozi mbalimbali
ili taarifa ziwafikie wananchi wote na waongezeke zaidi ya waliofika jana
Mama
Mwalukisa ni mfanyabiashara aliyekuwa mnadani hapo ambapo amesema ingawa
wananchi walikuwa wengi kiasi mnadani hapo lakini wamebaini kuwa taarifa
hazikufika ipasavyo kwa wananchi lakini pia kutokana na mnada huo kufanyika kwa
mara ya kwanza eneo hilo
huwenda nayo imechangia watu kutoshiriki kwa wingi
Akizungumzia
suala hilo
afisa biashara wilaya ya Makete Bw. Edonia Mahenge amesema wao walitangaza
matangazo hayo redioni pamoja na kwenye nyumba za ibaada lakini pia hawataacha
na badala yake wataongeza kasi ya matangazo ili taarifa ziwafikie wananchi wote