‘RAMA MLA WATU’ APELEKWA MIREMBE KWA UKICHAA


Stori:Richard Bukos
Kijana Ramadhan Seleman ‘Rama Mla watu’, aliyekuwa akishikiliwa na dola kwa tuhuma za mauaji ya mtoto, Salome Yohana licha ya kuondolewa hatia hiyo huku akiwekwa chini ya uangalizi baada ya kubainika kuwa na matatizo ya akili, Jumatano iliyopita alirudishwa hospitali ya waalifu ya Isanga iliyopo Mirembe, Mkoani Dodoma.

Rama alipandishwa basi ya Shukrani majira ya saa moja asubuhi akiwa na askari wawili waliokuwa wakimlinda kuhakikisha wanamfikisha kwenye hospitali hiyo, mpaka akili yake itakapotengemaa ndipo ataachiwa uraiani.

Kijana huyo alisafirishwa kupelekwa hospitalini huko kufuatia amri iliyotolewa na Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam katika kesi yake ya mauaji iliyokuwa ikiwakabili na mama yake, Khadija Musa, baada ya kubainika kuwa alitenda kosa hilo akiwa na matatizo ya akili.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo