Tarehe 20 Julai, 2013 kulitokea mauaji ya mfanyakazi wa mgodiwa Tanzanite ulioko kitalu
C, Mirerani wilayani Simanjiro kwakupigwa risasi na mchimbaji kutoka mgodi wa wachimbaji wadogowa kitalu D katika eneo hilo.
Kitendo hicho kimetokana na wachimbaji wadogo wanaopakanana Kitalu C kuvuka mipaka ya vitalu vyao na kuendesha uchimbajindani ya Kitalu C, jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Madiniya Mwaka 2010 na Kanuni zake.
Kwa sasa Kitalu C kinamilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Madinila Taifa (STAMICO) na Kampuni ya Tanzanite One kwa asilimia 50kwa 50. Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika.
Serikali haitavumilia kuona
Tunapenda kuwatangazia
Aidha, uchimbaji uzingatie taratibu za usalama migodini ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na utumiaji wa silaha za aina yoyote migodini. Ukaguzi wa migodi kubaini migodi inayoendeshauchimbaji ndani ya mipaka ya kitalu C utafanywa na Timu yawataalam wa Wizara ya Nishati na Madini. Vitalu vitakavyobainika kuhusika leseni zake zitafutwa na uchimbaji utatakiwa kusitishwakatika migodi hiyo.
IMETOLEWA NA,
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
26 JULAI, 2013