Picha ya Bwawa toka Maktaba.
Hatimaye Mwili wa Mwanafunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi
Matembwe Filbert Luwanja Umepatikana Katika Bwawa la maji Kijijini
Hapo,Ikiwa ni Zaidi ya Siku Tano Tangu Alipozama.
Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Itundu Bw Justin Mfugale Amesema Mwili Huo Umepatikana Jana Majira ya Saa Moja Jioni Baada ya Wakazi Wawili wa Kijiji Hicho Kuuona Ukielea Ikiwa ni Baada ya Jitihada za Muda Mrefu za Kuutafuta Mwili Huo.
Amesema Mazishi ya Mtoto Huyo Yanatarajiwa Kufanyika Leo Saa Saba Mchana Kijijini Hapo na Kuwaomba Wananchi Kuendelea Kushirikiana Katika Kukabiliana na Majanga Yanayojitokeza Kijijini Hapo.
Kwa Upande Wao Baadhi ya Mashuhuda na Wananchi Kijijini Hapo Wameiomba Serikali Kuongeza Nguvu Katika Uimarishaji wa Vitengo Vya Uokozi na Majanga na Ili Kuweza Kuokoa Maisha ya Watu Wakati Ajali Kama Hizo Zinazopotokea.
Mtoto Filbert Luwanja Alizama July 24 Mwaka Huu Majira ya Saa Nane Mchana Wakati Akiongelea na Wenzake Wawili Huku Wataalam wa Kuongelea na Kuzama Majini Wakionekana Kuwa Tatizo Sugu Mkoani Njombe .
Siku chache zilizopita mwaka huu wananchi wa mitaa ya Kibena walipatwa na simanzi ya kuzama kwa kijana mmoja Mexon Nyekelela Chota ambaye alizama kwenye bwawa la maji la kampuni ya Tanwat na hatimaye alipatikana baada ya siku Sita.
credit matukio na Ngilangwablog