Mtu
 mmoja anayetuhumiwa kuwa mmoja wa wawabakaji wabaya zaidi nchini Afrika
 Kusini Sifiso Makhubo (pichani) amekutwa amekufa katika sero ya gereza 
alilokuwamo.
Sifiso
 Makhubo ambaye alikuwa anakabiliwa na mashitaka 122 likiwemo la mauaji,
 mwili wake umekutwa saa chache kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi 
yake.
Pia
 alikuwa anashitakuwa kwa jaribio la kuua, kwa madai kuwa alikuwa 
akifahamu fika kuwa aliwaambukiza virusi vya ukimwi wale aliowabaka.
Afrika
 Kusini ina moja ya viwango vikubwa duniani vya matukio ya ubakaji, 
ambapo kwa mwaka uliopita kesi 64,000 ziliripoti polisi.
Pia
 ni nchi yenye idadi kubwa ya watu walioathirika kwa virusi vya ukimwi, 
ambapo watu milioni 5.5 sawa na asilimi 17 ya waathirika hao, wana umri 
kati ya miaka 15 hadi 49.
Mamlaka
 imesema Makhubo alikuwa mwenyewe katika sero hiyo na inaaminika 
alijinyonga kwa kutumia blanketi, hata hivyo wanachunguza mazingira ya 
kifo chake.
Alikuwa
 akishitakiwa kwa kuwabaka watoto 35 na wanawake wawili, kati ya Januari
 2006 na Februari 2011, huku mhanga mdogo kabisa akiwa na umri wa miaka 
10.