Nahodha
wa Taifa Stars Juma Kaseja yuko mbioni kwenda kukipiga katika klabu ya
FC Lupopo inayoshiriki ligi kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wakala wa klabu hiyo amesema tayari wameshakubaliana baadhi ya mambo na
mchezaji huyo na yamesalia masuala machache kabla ya Kaseja ambaye ni
mchezaji huru kwa sasa kujiunga na timu hiyo.