Na Ibrahim Yassin,Kyela.
KUFUATIA
ongezeko la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kuzidi kuongezeka wilayani Kyela
mkoani Mbeya asasi ya The Mango Tree inayojishughulisha na kulea watoto yatima
imetoa msaada wa dawa za kutibu maji kwa wakazi wa kata sita ambazo
zimeathirika zaidi na ugonjwa huo
Msaada huo
umekwenda sambamba na kuwapatia watoto yatima vifaa vya kusomea kama
Madaftari,kalamu,pencils,Free Style kwa watoto wa kike na vyandarua kwa ajiri
ya kuwakinga na ugonjwa wa maralia ambao pia bado unawasumbua watu wengi
wilayani Kyela
Akizungumza
wakati wa kukabidhi misaada hiyo katika kata za Bujonde na Ngonga kiongozi wa
mpango huo kutoka katika asasi hiyo ya The Mango Tree Bw,Obed Helly alisema
kuwa kama jamii itatumia vizuri dawa hizo za kutibu maji wana uhakika mkubwa wa
kupunguza kasi ya ugonjwa huo wa kipindupindu
Alisema
jamii inachotakiwa sasa ni kuhakikisha kuwa inazingatia kanuni za afya ikiwa ni
pamoja na kuzitumia dawa hizo ipasavyo na kuwa kutumia dawa ni rahisi zaidi
badala ya jamii kuchemsha maji na kuwa kila mmoja akitekeleza wajibu wake kila
kitu kinawezekana
Mkuu wa
idara ya elimu katika asasi hiyo Bw,Aloyce Mwakapotela alidai kuwa ipo haja kwa walezi
wanaowalea watoto yatima kuhakikisha kuwa wanavitunza vifaa hivyo wanavyopewa
ili viweze kuwasaidia watoto hao na kuwawezesha kupata elimu kama ilivyo kwa
watoto wengine
Taarifa za
idara ya afya zinaonyesha kuwa ugonjwa wa kipindupindu bado ni tatizo kwa maana
kuwa idadi ya wagonjwa wapya imekua ikiongezeka siku hadi siku ambapo mpaka
sasa wagonjwa waliopo ni 112 na huenda hari hiyo ikaendelea kutokana na ukaidi
wa watu kutofuata kanuni za afya kama wanavyoelekezwa na wataalamu wa afya
Kaimu mganga
mkuu wa wilaya Kyela Bi,Apaisaria Rumisha amesema kuwa kama wananchi wataziunga
mkono jitihada za serikali za kupambana na ugonjwa huo kuna matumaini makubwa
ya kuweza kuondokana na tatizo hilo lakini kama hari itaendelea hivyo basi
tatizo hilo litaendelea kuisumbua wilaya Kyela
Kutokana na
hari hiyo serikali ya wilaya imezuia mikusanyiko mbalimbali ya watu isiyokuwa
ya lazima,uuzaji wa vyakula na vyakula kutouzwa kwenye maeneo ya shule za
msingi na sekondari na mpaka sasa kuna baadhi ya watu wamekamatwa na kufikishwa
mbele ya vyombo vya sheria kwa makosa mbalimbali ya kukiuka sheria za kupambana
na ugonjwa huo