Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Junior Seminari inayomilikiwa na
kanisa la KKKT jimbo la Morogoro wamefanya mgomo wa kutoingia darasani
na kufanya maandamano kwenda ofisi za askofu kuukataa uongozi wa shule
kwa madai kushindwa kuweka huduma muhimu za taaluma na kuajiri walimu
wasio na uwezo wa kufundisha hali inayosababisha kushuka kwa kiwango
cha taaluma katika shule hiyo.
Ndivyo walivyosikika wanafunzi hao wakiimba nyimbo
za dini wakiandamana kuelekea katika kanisa la KKKT mji mpya huku askari
wa jeshi la polisi wakiyasimamisha maandamano kwa muda hadi alipofika
askofu wa jimbo la Morogoro Jacob Mameo ambapo maandamano yalielekea
kanisani na kabla ya mazungumzo kuanza walianza maombi kisha wanafunzi
wakakabidhi malalamiko yao kwa maandishi ambapo akijibu malalamiko hayo
askofu Maleo ameahidi kuyafanyia kazi ikiwemo kuitisha kikao cha bodi ya
shule kwa haraka.
Muda wote wanafunzi walionekana kutokuridhika na
majibu ambapo wameeleza kuwa malalamiko yao ni ya muda mrefu na kubwa
wanalolalamikia ni uwezo mdogo wa baadhi ya walimu katika kufundisha na
jingine wakilalamikia urasimu wa mwalimu mkuu wa shule hiyo Laison
Saming'o kushindwa kusimamia upatikanaji wa huduma za afya,vifaa vya
shule na usimamizi mbaya wa mitihani.
Nae katibu tawala wa wilaya ya Morogoro Sulpius
Mlenge akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Morogoro ameomba
askofu kutafuta ufumbuzi wa haraka wa malalamiko ya wanafunzi hao ili
yasiathiri taaluma zao na kuwasihi wanafunzi kutulia ambapo baadae
wanafunzi hao walirudishwa shuleni kwa daladala.
CHANZO:ITV