 |
| Mkurugenzi
wa Kampuni ya Steps, Diresh Solanki akimpa tuzo msanii bora wa kiume
katika tasnia ya filamu nchini Jacob Steven JB wakati wa utoaji wa tuzo
hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudhuriwa na wasanii wengi
nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa
zikitolewa kila mwaka.Picha na www.burudan.blogspot.com |
 |
| Pazia la Tuzo za Steps Bongo Movie Awards ukiwa umefunguliwa na waziri wa Sayansi na Teknolojia Makame Mbalawa |
 |
| Mzee Majuto akipokea Tuzo ya msanii bora wa uchekeshaji |
 |
| Msanii Steve Nyerere akipokea Tuzo |
 |
Msanii Nice Mohamedi 'Mtunis' akipokea tuzo ya Mwaka 2012 zilizoandaliwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya Steps Entertainment
|
 |
| MAMA SHILOLE AKIWA JUKWAANI |
 |
| Mtoto Jenifa akichukua tuzo yake |
 |
| Riyama akipokea tuzo yake |
 |
| Msanii Niva akichukua TUZO ya msanii bora Chipkizi kulia yupo msanii mwenzake Rado |
 |
Mjumbe
wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto
akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii
bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika
kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.burudan.blogspot.com |
 |
| Mjumbe
wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete wa tatu
kushoto akiwapongeza baadhi ya wasanii wa marehemu Kanumba baada ya
kuwakabizi tuzo
|
 |
| Mkurugenzi
wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akimkabizi tuzo ya mwongozaji bora
wa filamu nchini kwa mwaka 2012 Vicent Kigosi 'Ray ' wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia jana usiku. |
 |
| Mkurugenzi
wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akifafanua jambo baada ya kumkabizi
tuzo Vicent Kigos 'Ray' ya mwogozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka
2012. |
 |
| Wafanyakazi wa Kampuni ya Steps wakipokea tuzo |
 |
| Baadhi
ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo zao
za kwanza kwa mwaka 2012 zilizodhaminiwa na kampuni ya steps. |
 |
| MPIGA PICHA MOHAMED ARALAKIA ZA COVERS MBALIMBALI ZA KAMPUNI YA STEPS AKIPOKEA TUZO |
KAMPUNI ya
Usambazaji wa filamu ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam
mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa tuzo kwa wasanii bora waliofanya
vizuri katika tasnia ya filamu nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mara
ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo hizo
Akizungumzia tuzo hizo
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Direshi Solanki amesema kuwa tuzo hizo
watakuwa wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini
kampuni hiyo iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka
historia ya kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo
Baadhi ya
washindi ambao waliopatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni
Steven Mangendela 'Steve Nyerere', Issa Mussa 'Cloud 112' Mohamed
Nurdini 'Chek budi' Nice Mohamed 'Mtunisi' Irene Paul akinyakuwa msanii
bora chipukizi wa kike
Wakati katika kinyanganyiro cha kumpata
msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob Steven 'JB' huku msanii bora wa
kike ikienda kwa mwana dada Irene Uwoya, na msanii bora wa filamu za
mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda 'Jimmy Masta'
Wakati katika kipengele cha muongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent Kigosi' Ray' na kampuni yake ya RJ Filamu
Mbali
na hivyo kulikuwa na tuzo za heshima kwa wasanii waliofanya vizuri
lakini kwa sasa hawapo duniani moja ni kwa Steven Kanumba, Juma Saidi Kilowoko
'Sajuki' John Stefano, Hussein Ramadhani Mkiety 'Sharo Milionea'
Katika utoaji wa tuzo hizo kulikuwa na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi