
Akizungumza Mkurugenzi wa mawasiliano wa idara ya
sheria Bi ELIZABETH NZANG katika semina hiyo iliyofanyika katika
chuo kikuu huria Manispaa ya Iringa, amesema kuwa mamlaka inahimiza wadau wote
waliochukua leseni na watakaoomba leseni kufuata sheria kwani kwa kutofanya
hivyo mamlaka itamtoza faini , itamfungia kituo au adhabu ya kifungo.
NZANGI amesema kuwa ukiukwaji wa sheria mamlaka inayo wajibu
kuwaadhibu huku akitaja aina za leseni kuwa kumiliki na kujenga miundombinu,
kuendesha na kuunganisha mawasiliano,kutoa huduma za masiliano ,leseni za
maudhui , vifaa vya mawasiliano, leseni za very small aperture terminals pamoja
na utumiaji wa vifaa vya masafa.
Mbali na suala hilo la leseni mamlaka pia inatoa taarifa kuanzia
july mosi yeyote ambaye atanunua simu ambayo haijasajiliwa haitotumika na
kusema kuwa unaposajiliwa hakikisha kwa namba inayianzia nyota mia
na sita leri ili kuhakikisha kama usajili umekamilika.
Aidha Mamlaka inaomba wananchi kutoa ushirikiano ili waweza
kufanya kazi vizuri kwa mujibu wa sheria namba 21 huku ikiwaonya watanzania
kutonunua simu kwa wamachinga na kuahidi kushughulikia malalamiko kwa haraka
likiwemo la utumiaji wa mabadiliko ya fedha .