Kutokana na kukitihiri kwa kero ya maji katika kata ya Nduli
maeneo ya njia panda ya Mgongo Manispaa ya Iringa, wananchi wameutupia lawama
uongozi wa kata hiyo kwa ukosefu wa huduma kwa kipindi kirefu.
Wakizungumza na mapema leo,wakazi hao wa kata ya NDULI maeneo ya
njia panda ya Mgongo, wamesema kuwa inawalazimu kutumia maji ya madimbwi kwa
miaka mingi na tayari michango kwa ajili ya kuleta huduma hiyo ya maji
imekwisha changwa.
Akijibia lawama hizo Diwani wa kata ya nduli mh. Rashidi
Chonanga amekiri kuwepo kwa tatizo la maji katika kata yake na sasa
wanamtafuta mkandarasi wa maji ili kuhakikisha maji yanafika maeneo yote ya
Nduli.