Watu
saba wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kufanya fujo
katika chaguzi ndogo za udiwani katika wilaya ya kilolo na mufindi huku
likimshikilia mtu mmoja aitwaye Saadat Daud kwa kosa la uchochezi.
Akizungumza
na wandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Iringa,Ramadhani Mungi,
mnamo tarehe 15 mwezi huu majira ya saa 7 mchana katika kijiji cha
ng’ang’ange wilaya ya kilolo Runyiliko Nyaulingo (60) alifika katika
eneo la CCM,wakifamya maandalizi ya mkutano wa kampeni na kuwafanyia
fujo.
Kamanda
amesema kufuatia fujo hizo wafuasi wa ccm walimpiga na kumjeruhi mkono
kitendo kilichopelekea wafuasi wa CHADEMA wakiwa na marungu na mapanga
walikwenda kumuokoa mwenzao lakini polisi waliwahi kufika kutuliza fujo
na wanamshikilia WILHADI NGOGO 40 inasemekana kuwa ni mfuasi wa chadema.
Kamanda
pia majira ya saa 5 wafuasi wa chadema walikuwa wakifanya kampeni za
nyumba kwa nyumba walifika katika kijiji cha maguvani kwenye nyumba ya
LUSTIKA MHELELE gafla walifika watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa ccm
na kumshambulia kwa kitu chenye ncha kali DANIEL EDSON 45 na katika
tukio hilo wanamshikilia YOHANES MCHAFU 45.
Amesema
kuwa baada ya kujeruhiwa kwa DANIEL EDSON wafuasi wa chadema walifunga
barabara ya mbeya iringa kwa magogo wakiongozwa na kiongozi wao aitwaye
SAADAT DAUD na fujo hizo zilitulizwa na jeshi la polisi.
Aidha
ameongeza kwa kusema kuwa mnamo tarehe 16 majira ya saa 11 jioni
waliwakamata watu watatu wafuasi wa chadema wakiwa na mapanga na
misumari katika kijiji cha ukemele kata ya mbalamaziwa DAMIANI OMARI 18
amemaliza kidato cha nne katika shule ya sekondari sangu mkoani mbeya
JOSEPH MWAKATO 17 mwanafunzi kidato cha pili sinde sekondari pamoja na
GEORGE MYAO 32 mpishi wa tazara ambaye pia ni katibu wa BAVICHA.
CREDITS:JIACHIE