Moto mkubwa uliowaka baada ya ajali mbaya ya barabarani iliohusisha lori
la mafuta, umewauwa takriban watu 33 mjini kampala Uganda. Watu wengine
30 wanadaiwa kujeruhiwa vibaya kufuatia tukio hilo.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa kati ya waliofariki ni raia waliokuwa
wanakimbilia eneo hilo la mkasa kuteka mafuta yaliokuwa yakivuja kutoka
kwa lori hilo.
maafisa wa serikali walikuwa katika harakati za kutambua mili ya waliofariki baada ya wengi wao kuchomeka vibaya.
Idara
ya polisi imesema kuwa waliofariki waliteketea kiasi cha kutotambulika
na itabidi watumie utaalamu wa vinasaba au DNA kutambua miili ya
waliokufa. Source: BBC