Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Ludovick Utouh.
Na.Eleuteri Mangi- Maelezo
Tanzania
kupitia Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imetiliana saini
mkataba wa Euro 3,500,000 na Shirika la Deutsch Gesellschaft fü
Internationale Zursammenarbeit (GIZ) la nchini Ujerumani ambazo ni sawa
na shilingi Bilioni 3,750,000,000/= za kitanzania kwa ajili ya kusaidia
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza
mbele ya Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Ujerumani,
Wafanyakazi wa NAOT na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam hivi
karibuni Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Ludovick Utouh
amesema makubaliano hayo yanalenga kusaidia miradi iliyopo katika ofisi
yake.
“Mara
kwa mara ofisi yangu imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi katika
maeneo mbalimbali ya kiutendaji hivyo makubaliano haya yataisaidia ofisi
hii kufanya kazi kiufanisi zaidi na kwa kuzingatia weledi,” amesema
Utouh.
Utouh
alifafanua kuwa ofisi yake ina jukumu kubwa na la muhimu la
kuhakikisha kuwa kuwa rasilimali za nchi zinatumika vema na kwa manufaa
ya kila mtanzania hivyo fedha hizo zitatumiaka kwa manufaa ya nchi
nzima.
Naye
Mkurugenzi wa GIZ nchini Dkt. Regine Qalmann alisema shirika lake
litaenelea kushirikiana na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Tanzania kwa nia ya kudumisha mihusiano yaliyopo kati ya nchi hizo
mbili.
Makubaliano hayo kati ya Serkali ya Tanzania na Ujerumani yatadumu kwa muda wa miaka mine kuanzia mwaka huu wa fedha.