
Rapper
Ney wa Mitego, kupitia wimbo wa "Nasema nao" alifanikiwa kupata tuzo ya
wimbo bora wa hiphop, ambao umesababisha malalamiko kwa baadhi ya
wasanii wengine ambao wnaona hakustahili kuchukua tuzo hiyo kwa wimbo
huo, huku wengine wakidai Fid q anastahili na wengine kudai Stamina ndio
anastahili....leo hii Ney mwenyewe kafunga juu ya swala hilo
"aah wasanii
ndio wanaolalamika na wameandika kwenye mitandao, lakini mwisho wa siku
lazima tukubali matokeo kwamba mziki unabadilika kila kukicha, mi
nawaambia wasanii wenzangu kwamba mkiendelea kung'ang'ania huko mtakufa
njaa, halafu mwisho wa siku wataendelea kulia tu kila siku kwamba kuna
hili mara lile,mi naimani kwamba mashabiki wangu ndio wamenikabidhi
tuzo, media zinazosapoti kazi yangu ndio zimenisaidia mpaka mimi
nimezungumza na mshabiki wangu popote walipo mpaka juzi nimepata tuzo ya
wimbo bora wa hiphop.
mi nastahili kupata tuzo, kwasababu kwanza sijui
wao wanafanya hiphop gani, wakae waeleze mziki wao wao ni hiphop
kwasababu hii na hii na hii na wangu sio hio hiphop kwasababu hii na hii
na hii. bwana hiphop ni ukweli na unabadilika kila siku kila kukicha.
Mi nawashauri tu kitu kimoja, sitaki kubishana na msanii yoyote, wana
njaa, wakiendelea kung'ang'ania huko watakufa njaa, kwanini watu
wamemsapoti Ney, kwanini watu wamemsapoti Kala Jeremiah,angalia mashairi
ya Kala yako wazi, lakini we unaweka sijui mafumbo ya dizaini gani nani
atakuelewa...........
halafu tuzo sio lazima upate tuzo, sio lazima ulaumu, kuna wasanii
wakali hawajawahi kupata tuzo lakini hawajawahi kulalamika, kuna wasanii
kama Juma Nature, nani anaweza kusimama stage na Nature? sijawahi
kumsikia anaongea.....
category moja tu nimewekwa nimetusua wao wanalia, shauri yenu shauri
yenu, jipangeni mwakani, mi staki kubishana nao, am the best, halafu
wasipoangalia nawatengenezea kiwanda kwa ajili ya kuwaajiri
wanapoendelea kuwana na hali ngumu, natengeneza kiwanda ambacho
ntawaajiri wasanii wanaofeli wote kwasababu hawana shughuli za
kufanya." amesea Ney.