Wakazi wa
kata ya Elerai ,Arusha mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye mara baada ya kufungwa kwa kampeni za
uchaguzi wa Diwani, juni 14.2013.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na wanachama wa CCM kata ya Elerai mara tu baada ya
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akibadilishana jambo na mmoja wa
wanachama wakongwe wa kata ya Elerai kabla ya kuanza kwa mkutano wa
kufunga kampeni za uchaguzi wa Udiwani ya kata hiyo.
Mbunge
wa Vijana mkoani Arusha , Ndugu Catherine Magige akihutubia wakazi wa
kata ya Elerai na kuwataka wakazi wa kata hiyo kutambua thamani ya kura
kwa kuichagua CCM.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Mhe. Goodluck Olemadeye akihutubia wakazi wa kata ya
Elerai na kuwaambia CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi kwa wakati na
kila kilichoahidiwa Arusha kitafanyika.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa kiti cha
udiwani kata ya Elerai, Mwl.Emmanuel Laizer,na kuwaambia wana Arusha
muda wa kufanya maendeleo ni huu na CCM haina kazi nyingine zaidi ya
kuleta maendeleo Arusha.
Mgombea
wa kiti cha Udiwani kwa tiketi ya CCM, Mwalimu Emmanuel Laizer
akihutubia wakazi wa kata ya Elerai kwenye mkutano wa kufunga kampeni.
Bibi
na mjukuu wake wakifuatilia kwa makini yale yanayosemwa na viongozi wa
CCM wakati wa kufunga kampeni za udiwani kata ya Elerai.
Mbunge wa
Vijana Arusha ,Ndugu Catherine Magige akisikiliza kwa makini sera za
mgombea wa udiwani wa kata ya Elerai ,Mwl. Emmanuel Laizer.
Mboya
akihutubia wakazi wa kata ya Elerai na kuwaelezea kuwa alipotea sana
kuishabikia Chadema na amewasihi wakazi wa kata hiyo kutofanya makosa
kama kweli wanataka maendeleo.









