Jitihada zinazofanywa na asasi ya ELCT Makete kupitia program
yake ya Pamoja Tuwalee zimeendelea kuzaa matunda baada ya hivi karibuni kuwaibua
watoto wawlili wa kata ya Ipelele wilayani Makete ambao wanaishi katika
mazingira hatarishi zaidi na kuweka matatizo yao kwa jamii ili iwasaidie
Jitihada hizo zilizaa matunda kwa watoto hao Zaifa Daudi na
Nobi Sadiki (PICHANI JUU) ambapo mkuu wa wilaya ya makete Bi Josephine Matiro ameahidi
kuwasaidia watoto hao sare za shule kwa kipindi chote atakachokuwepo kwenye
wilaya hiyo
“Ndugu zangu nimeguswa sana na maelezo ya watoto hao ambao
wanaishi katika mazingira hatarishi, wanadiriki kufanya vibarua ili wazilee
familia zao ukizingatia watoto hawa ni yatima, mimi naomba suala la uniform (sare)
za hawa watoto niulizwe mimi mpaka nitakapotoka Makete
Kwa mujibu wa Mratibu wa program ya pamoja Tuwalee wilayani
hapo Mchungaji Ezekiel Sanga, watoto hao mmoja wao anasoma darasa la tatu na
amamlea bibi yake ambaye ni mzee sana ambapo mtoto huyo hulazimika kutafuta
vibarua na kuvifanya ili apate fedha za kujikimu yeye na bibi yake huku mtoto
mwenzake naye akishirikiana na dada yake kufanya vibarua ili wajikimu kumaisha
Mchungaji Sanga amesema pamoja na ukosefu wa sare za shule
walionao watoto hao lakini pia malazi yao ni tabu, na wakati mwingine
wanashindwa kuhudhuria masomo yao kwa kuwa hulazimika kwenda kutafuta vibarua
vya kufanya huku akiitaka jamii inayowazunguka watoto hao kuona umuhimu wa
kuwasaidia kwani watoto hao hawakupenda kuishi maisha hayo magumu waliyonayo
mara baada ya kufiwa na wazazi wao
Hivi majuzi wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika
watoto hao walichangiwa zaidi ya sh. 282,500 lakini pia hamasa ikawekwa kwa
jamii inayowazunguka watoto hao kuwasaidia kwa mahitaji yao ili watoto hao
waishi kwa raha
Programa hiyo ya pamoja tuwalee wilayani hapo imekuwa
ikiibua changamoto wanazokumbana watoto na kuziweka wazi ikiwemo kuwatafutia
ufumbuzi wa matatizo yanayowakumba watoto hao kwa kuwashirikisha wadau kuona
matatizo hayo ni ya kila mtu
Na Edwin Moshi