SERIKALI Imetoa kiasi cha fedha sh milioni 100
ambacho itamzawadia mtu atakaye mfichua aliyerusha bomu katika mkutano
wa kampeni za udiwani za CHADEMA Mkoani Arusha.
Kiasi hicho cha fedha
kimetangazwa muda huu bungeni mjini Dodoma ili kuhakikisha inachochea
kupatikana kwa mtu huyo.
Hata hivyo Serikali imeahidi kumsaka mtu huyo anayedaiwa kurusha bomu
ambalo limesababisha kufa kwa watu wawili hadi sasa na wengine zaidi ya
70 kujeruhiwa.
