Bi Mery Mbilinyi ambaye ni diwani viti maalumu tarafa ya Lupalilo wilayani Makete ambaye kwa hivi sasa anasubiri adhabu yake kutoka CCM mkoa wa Njombe
Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilaya Makete Jasel Mwamwala ambaye amepewa onyo kali
Katibu wa ccm wilaya ya Makete Miraji Mtaturu akitoa taarifa kwa waandishi wa habari
==========
Chama cha mapinduzi wilayani Makete kimewavua
madaraka viongozi kadhaa wa chama hicho na wengine kupewa muda wa
maangalizo wakiwemo makatibu na
wenyeviti wa matawi na
diwani wa viti maalumu Bi: Mary Mbilinyi ambaye bado anasubiri uamuzi kutoka katika ngazi ya mkoa ya chama
chama cha mapinduzi
Akitoa taarifa kwa
vyombo vya habari katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya
Makete Bw Miraji Mtaturu
Alisema kuwa adhabu hiyo
kwa viongozi hao Imetolewa baada ya kujadiliwa
katika kikao cha kamati ya
maadili na usalama cha chama hicho na kupitshwa na kikao cha kamati ya siasa ya kilichofanyika
hapo juzi na ndipo kuamua kutoa taarifa
hiyo kwa umma kwini viongozi hao wamekuwa wakivunja sheria na taratibu za chama
hicho cha siasa wilayani Makete
“Katika kikao cha kamati ya maadili na usalama ya viongozi wa chama cha mapinduzi
kilichofanyika tarehe kumi na tatu
mwezi juni kilijadili mienendo na tabia za baadhi ya wananchi na viongozi na kupitishwa na kikao cha kamati
ya siasa waliobainika kuvunja sheria
waliitwa na kujibu tuhuma zao na sisi tukajitosheleza na kuamua kuchukua
uamuzi kama ofisi ya chama ngazi ya
wilaya” alisema katibu huyo.
Akiendelea kuongea na Vyombo vya habari katibu Huyo Aliwataja viongozi ambao wamevuliwa madaraka kutokana
na kukosa sifa ya kuwa viongozi baada ya
Kukiuka maadili ya chama hicho kuwa ni
katibu wa tawi la Luvulunge
lililopo katika kata ya Isapulano
Wilayani Makete Bw. Festo Chaula
na katibu wa tawi la Mago
lililopo katika Kata ya Lupalilo
Bw.Creto Ngomano.
Aliwataja Viongozi waliopewa onyo na Kupewa Muda wa angalizo la
miezi sita kuwa ni pamoja na mwenyekiti wa kijiji cha Luvulunge Bw. Daudi Mwamkinga na kiongozi mwingine
ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Bw Jasel Mwamwala na kuongeza kuwa kiongozi huyo alikiri katika
kikao cha kamati hiyo na ripota wetu alipopata taarifa hii alimtafuta kwa njia
ya simu naye ailikana kuwa na taarifa ya kupewa onyo na chama hicho.
Pia Katibu huyo alimtaja diwani wa viti maalumu Katika chama cha mapinduzi wilayani
Makete Bi. Mary Mbilinyi kuwa ni
miongoni mwa viongozi ambao wamekuwa
wakivunja maadili ya chama hicho cha
mapinduzi ambaye bado anasubrli uamuzi
utakaoendana na adhabu utakaotangazwa na chama hicho ngazi ya mkoa wa Njombe
Aidha aliwataka viongozi wa chama hicho kuwa makini katika utendaji wao wa kazi na
kusema kuwa chama cha mapinduzi kina mtandao mrefu hivyo kina uwezo mkubwa wa kuwakamata viongozi ambao wanakiuka katiba ya chama hicho.
“Nawakubusha viongozi wa chama cha mapinduzi kwamba chama cha mapinduzi kina mkono
mrefu kinafika hadi katika ngazi ya
matawi na shina na kwamba mtu yeyote ataweza
kuukwepa mkono wa chama hichi
asiwezekurekebishwa ni jambo
lisilowezekana “ alisema katibu huyo
Akizungumzia suala la mchakato wa katiba katibu huyo
aliipongeza tume hiyo kwa ufanyaji wa kazi mzuri hadi uwasilishwaji wa rasimu hiyo ya katiba
na kuwaunga mkono baadhi ya viongozi wa chama chake katika kipengere cha kuwepo kwa maraisi
watatu na kusema kuwa kujiongezea
gharama zisizo na msingi
“Naipongeza tume ya katiba chini ya Jaji mstaafu Warioba
kwa kazi nzuri walioifanya hadi
walipofilkia Lakini maoni ni ya kila mtu
anaweza toa na kuhusu suala la kuwa na maraisi watatu hilo hata mimi
nalipinga kwani ni kujiongezea gharama
na jambo lingine ni suala la serikali ya shirikisho hakuna sababu ya kuwabebesha mzigo watanzania na vyama vya siasa….." alisema
katibu huyo.
Na James Festo
